.RU

Amani kwa ukristo ulio wa kweli - старонка 18


NDOAMbali na Suleimani kuanza vyema, wakati bado kabisa akingali kijana alifanya makosa ya mintarafu ya ndoa ambayo kwa kuyaendekeza yalinyonya nguvu zake za kiroho alipozeeka. "Mfalme Suleimani akawapenda wanawake wengi wageni …… wanawake wa moabu, na wa Waamoni, na Waedomi …. Na wa mataifa Bwana alivyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu: kwa kuwa hakika watageuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Suleimani akaambatana nao kwa kuwapenda …. Wake zake wakamgeuza moyo wake. maana ikawa Suleimani alipokuwa mzee, Wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, ….. Suleimani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana,wala hakumfuata Bwana akamghadhibikia Suleimani …. Kwa hiyo Bwana akamwambia …. Hakika nitaurarua ufalme usiwe wako"

(1Fal. 11: 1 -11).Kuteleza na kuiacha imani Suleimani kulidumu maisha . Uhusiano wake na wanawake ambao hawakushiriki maarifa yake kwa Mungu wa Israeli kulimwongoza kuwa na uhusiano wa kuielekea miungu yao ya uongo. Upendo wake kwa wake zake ilimaanisha hakuona tena miungu hii inamkengeusha kiroho toka kwa Mungu wa kweli ambapo ndivyo ilikuwa. Kadri muda ulivyosonga mbele , moyo wake haukumwabudu tena Mungu wa Israeli."Moyo wake haukutimilika"yaani, dhamira yake haikumchoma tena kuabudu miungu inayodanganya. kukosa moyo wake wote kujitoa kwa Mungu wa kweli "ukawa ni uovu machoni pa Bwana"ikasababisha Mungu kuvunja uhusiano na Suleimani. Israeli waliambiwa mara kwa mara wasioane na wanawake wa mataifa yanayowazunguka

(Kut. 34: 12 -16; Yoshua. 23: 12, 13; K/Torati 7:3).Kwa kubatizwa katika Kristo kiroho tunakuwa Israeli, kama hatujaoa, tuoe tu ndani ya Israeli kiroho,"Katika Bwana"

(1Kor. 7:39)

- yaani, mwamini mwingine aliyebatizwa 'Katika Kristo’ Ikiwa tayari tumeoa wakati tunabatizwa, tusitengane na wake zetu; uhusiano wetu wa ndoa unatakaswa kwa sababu ya imani yetu (

1Kor. 7: 12 -14).

Kwa kufahamu, kuchagua kuoa wale ambao hawamjui Mungu wa kweli, kwa muda mrefu, watatuongoza kwenye ukengeufu wetu. Solomoni ni dhahiri alishindwa kukubali onyo la nguvu za Mungu kuhusu wanawake hawa:"Hakika wataugeuza moyo wako"

(1Fal. 11: 2; Kut. 34: 16

). Usawa pekee wa ajabu wa kujiweza na nguvu ya mawazo ya toba inaweza kutufanya tusihesabiwe na amri hii .

Awali tumeonyesha jinsi huo Ukristo wa

orthodox

haukubali msingi wa Wayahudi ambao ni tumaini la mkristo; hawamjui Mungu wa kweli wa Israeli. Kuoana na watu hawa wasiomjua Mungu kutatupeleka pole pole kutofautiana na utukufu wenye kweli ya mafunzo ambayo ni msingi wa wokovu wetu. Kwa sababu hii Isaka na Yakobo walikwenda umbali wa ajabu kuoa wanawake ambao waliishika imani ya kweili vema, Isaka akasubiri mpaka alipofikia umri wa miaka 40 ili kupata mke anayefaa

(Mwa. 24: 3, 4; 28: 1).

Sababu iliyoleta huzuni kwa Ezra na Nehemia waliposikia ya kuwa Wayahudi wengine walioa wasio wayahudi zaidi inaonyesha ukubwa wa toleo hili

(Ezra. 9:12; Nehemia 10: 29, 30).

Tumeleta jambo hili kwenye hatua hii ili kusaidia kufikiri kwa kuangalia; ndoa imejadiliwa kwa maelezo zaidi katika

somo la 11.4.HUKUMU YA MUNGUYakiwa ni matokeo ya kukengeuka Suleimani, Ufalme wa Israeli ukagawanyika na kuwa falme mbili; mwanae Suleimani,Rehoboamu, akatawala juu ya kabila ya Yuda, Benjamini na nusu ya kabila la Manase, wakati Yeroboamu akatawala juu ya kabila zingine kumi. Huu ufalme wa kabila kumi uliitwa Isrraeli,au Efraimu, ambapo makabila mawili yaliitwa Yuda. Watu wote wa kabila hizi kwa sehemu kubwa walifuata mfano mbaya wa Suleimani - walidai kumwamini Mungu wa kweli, wakati huo huo wakiendelea kuziabudu sanamu za mataifa waliowazunguka. Mara kwa mara Mungu aliwasihi, kwa njia ya manabii, ili watubu, bali haikufaa. Kwa sababu hii akawaadhibu kwa kuwatoa kwenda nje ya ufalme wa Israeli waingie nchi za adui zao. Hii ilikuwa kwa waashuri na wakaldayo wakiihusuru Israeli na kutwaa mateka. "Miaka mingi (Mungu) akachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako (neno) kwa vinywa vya manabii wako: (bali) wao wasitake kusikiliza; kwa hiyo ukawatia katika mikono ya watu wa nchi (zilizowazunguka)"

Nehemia 9:30

.

Kabila kumi, ufalme wa Israeli, haukuwa na wafalme wazuri hata kidogo. Yeroboam, Ahazi, Yehoahazi n.k wote wameandikwa taarifa zao katika kitabu cha wafalme wakiwa ni waabuduo sanamu. Mfalme wao alikuwa Hoshea, kipindi cha utawala wake Israeli walipopigwa na waashuri, nao kabila kumi wakachukuliwa utumwani

(2 Fal. 17)

. kutokana na hii hawakurudi kamwe .

Ufalme wa Yuda wenye kabila mbili ulikuwa na baadhi ya wafalme wazuri

(k.m Hezekia na Yosia)

, ingawa walio wengi walikuwa waovu. Kwa ajili ya watu kurudia -rudia kutenda dhambi, Mungu akaupindua ufalme wa Yuda katika kipindi cha utawala wa mfalme wao wa mwisho, Sedekia. Hsii ilitokana na wao kuvamiwa na wakaldayo , waliowachukua kwenda utumwani Babeli

(2 Fal. 25)

Walibakia Babeli kwa miaka 70, Wengine wakarudi baadae Israeli chini ya uongozi wa Ezra na Nehemia. hawakuwa tena na mfalme wao, walipokuja tawaliwa na wakaldayo, wayunani na warumi. Yesu alizaliwa wakati wa kipindi cha utawala wa Warumi. Kwa sababu ya Israeli kumkataa Yesu, Waroma wakawavamia mwaka 70 B.K na kuwatawanya ulimwenguni pote. Ni miaka 100 tu iliyopita walianza kurudi, hii ni ishara inaonya kurudi kwa Kristo
{ Ona kilichotiwa mwishoni mwa kitabu sehemu ya 3 }

{ nyongeza iliyotiwa mwishoni mwa kitabu}.

Ezekieli 21: 25 -27

mistari hii ilitabiri mwisho wa ufalme huu wa Mungu kama ulivyoonekana katika taifa la Israeli: "Na wewe, Ewe mtu mwovu, uliyetiwa jeraha kiasi cha kuwa , Mkuu wa Israeli (yaani, Sedekia), ambayo siku yako imekuja ….. Bwana

MUNGU

asema hivi; Kiondoe kilemba, ivue taji; (yaani Sedekia atakoma kuwa mfalme) haya hayatakuwa tena kama yalivyo; …… Nitakipindua, hiki nacho Nitakipindua, Nitakipindua, hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa"Maneno baada ya maneno kwa manabii wanaohuzunikia kukomeshwa kwa ufalme wa Mungu

(Hos.10: 3; Omb. 5:16; Yer. 14:12; Dan. 8: 12 -14).‘Kupindua’ mara tatu iliyo katika

Ezekiel 21: 25 -27

unatajwa uvamizi uliofanywa mara tatu na Nebukadneza, mfalme wa Babeli. Mwanafunzi anayekesha ataona katika mistari hii mfano mwingine wa jinsi ufalme wa Mungu na mfalme wake anaweza kutendwa sawa; Kuangushwa kwa Sedekia ulikuwa huo ufalme wa Mungu (ona sehemu ya 5:2). Hivyo ufalme wa Mungu kama ulivyokuwa katika taifa la Israeli ulifika mwisho: "….. na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli"

(Hos. 1:4)

, "Hiki nacho hakitakuwa tena , hata …."Inaleta kidokezo kwamba ufalme utaanza tena hapo"atakapokuja ambaye ni haki yake; naye (Mungu) atampa”. Mungu atampa (Yesu) kiti cha enzi cha Daudi Baba yake ….. na ufalme wake hautakuwa na mwisho"

(Luk. 1: 32, 33) -

Kristo akirudi. Basi, hii ni hapo ahadi ya kurudishwa ufalme itakapotimizwa.

KUTENGENEZWA KWA ISRAELILipo jambo kubwa lililoandikwa katika Agano la Kale lote na manabii la kurudishwa ufalme wa Mungu akirudi masihi.Wafuasi wa Kristo walielewa vema hili:"Basi walipokutanika, wakamuuliza, wakisema, Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme ?"yaani, '

Unabii wa Ezekieli 21:27

utatimia sasa ?’ Yesu alijibu kwa kusema kuwa muda hasa wa yeye kuja mara ya pili hawata ujua, Ingawa malaika haraka baadaye waliwahakikishia kuwa atarudi wakati fulani (

Matendo. 1: 6 -11).Kutengenezwa ufalme wa Mungu / Israeli kutakuwa basi akirudi mara ya pili. Hivi Petro alihubiri ya kuwa Mungu atamtuma "Yesu Kristo

…….. ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni (yaani, asalie kule) hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu"

(mdo. 3:20,12)

. Kuja mara ya pili kutafanya uanzishwe tena ufalme wa Mungu kama kutengeneza tena ufalme wa Israeli wa zamani.

Kwa kweli kutengeneza tena ufalme wa Mungu ni msemo wa"Manabii wote watakatifu wa (Mungu)”:-

 1. “Kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema: na mmoja (

  Yesu

  ) ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi (akija mara ya pili -

  Luk. 32,33

  ), akifanya hukumu …… mwepesi wa kutenda haki"

  (Isa. 16:5)

  .
 1. “Siku hiyo nitainua tena masikani ya Daudi yaliyoanguka (yaani, kiti cha enzi cha Daudi kilichosemwa na

  Luk.1: 32,33)

  , na kuziba mahala palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale"

  (Amosi. 9:11

  . Fungu la mwisho la maneno ni Lugha iliyowazi ya kutengeneza tena.

 2. “Watoto (Israeli) wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu"

  (Yer. 30:20)

  .
 1. “Bwana atachagua Yerusalemu tena"

  (Ezek. 2:12)

  , atafanya mji mkuu kwa ufalme wake wa ulimwengu wote

  (Zab. 48:2; Isa. 2:2 -4)

  .
 1. “Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza ……. Itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe ……. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi kama kwanza ….. katika mahali hapa

  (Yerusalemu

  ) ….. yatakuwepo makao ya wachungaji …. Makundi ya kondoo yatapita"

  (Yerusalemu

  33: 7 -13).Kurudi kwa Kristo kuanzisha huu ufalme kwa kweli ni "tumaini la Israeli”, ambalo yatupasa tujihusishe kwa kubatizwa.

5.4 Ufalme wa Mungu kwa Wakati UjaoSehemu ya 1 na 3 ya somo hili zimetoa habari kiasi cha kutosha kuhusu jinsi huu ufalme utakavyokuwa. Tumeona kuwa Abrahamu aliahidiwa kwamba kwa njia ya mzao wake watu toka maeneo yote ya ulimwengu watabarikiwa;

Rum.4: 13

inapanua suala hili kuwa na maana ya kuwa Dunia yote itakaliwa na hao watu ambao wamo'Katika’ Uzao wa Abrahamu, yaani Kristo. Unabii ulio katika sanamu ya

Dan. 2

waeleza Kristo atakavyorudi kama jiwe dogo, na kisha pole pole ufalme utapanuka na kuwa wa ulimwengu wote

(Zab.72:8).

Hii inamaana ya kwamba ufalme wa Mungu hautakuwa eneo la Yerusalemu pekee au katika nchi ya Israeli , kama wengine wanavyosema, kama maeneo haya hakika yatakuwa maeneo yake makuu. Wanaomfuata Kristo katika maeneo haya watakuwa"Wafalme na makuhani; tutatawala dunia"

(Uf. 5:10).

Tutakuwa wasimamizi juu ya makazi ya watu ya ukubwa mbali mbali na idadi; mmoja atakuwa juu ya miji kumi, na mwingine juu ya mitano

(Luk. 19:17)

. Kristo atashiriki utawala wake pamoja nasi

(uf. 2:27; 2 Tim 2:12)

."Mfalme (Yesu) atamiliki kwa haki, na wakuu (

Waaminio

) wake watatawala kwa hukumu"

(Isa. 32:1; Zab. 45: 16).Kristo atamiliki milele katika kiti cha enzi cha Daudi kitakachokuwa kimewekwa tena

(Luk. 1: 32, 33)

, yaani, atakuwa na mahali pa Daudi na cheo cha utawala, kilichokuwa Yerusalemu. Ikiwa Kristo atamiliki tokea Yerusalmeu, Huu utakuwa ni mji mkuu wa ufalme ujao. ni kwenye eneo hili ambapo hekalu litajengwa

(Ezek. 40 -48)

. Wakati watu watamtukuza Mungu sehemu mbali mbali za ulimwengu wote

(Malaki. 1:11)

, Hekalu hili litakuwa kitovu cha ibada walimwengu. Mataifa"watakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu mfalme, Bwana wa majeshi, na k ushika sikukuu ya vibanda"kuzunguka hekalu katika mji wa Yerusalemu

(Zekaria 14:16

). Hii hija ya mwaka kwenda Yerusalemu pia imetabiriwa kwa

Isa. 2: 2,3) "

Katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana

(Ufalme- Dan.2:35,44)

wa nyumba ya Bwana (Hekalu) utawekwa imara juu ya mlima (yaani, ufalme wa Mungu na hekalu vitawekwa juu ya falme zetu) ….. na mataifa yote watauendea makundi makundi Na mataifa wengi watakwenda na kusema, Njooni twendeni juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atafundisha njia zake, ….. maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu" Hii inaonekana kuwa picha ya siku za kwanza za ufalme, watu walipotangaza maarifa ya miliki ya Kristo kwa wengine, na watu wanakwenda juu "Mlimani"wenye ufalme wa Mungu, ambao utaene taratibu ulimwenguni pote. Hapa tuna picha ya shauku ya kweli katika ibada ya dini .

Moja ya mambo makubwa yaletayo huzuni kwa mwanadamu wa siku zetu ni kwamba watu'humwbudu’ Mungu kwa siasa, kwa makundi kukaa pamoja , kwa mazoea au kwa hangaiko la moyo, kuliko juu ya msingi wa ufahamu wa kweli kwake akiwa ni Baba yao na muumba. Katika Ufalme kutakuwepo shauku ulimwenguni pote ya kujifunza njia za Mungu; watu watakuwa na nia ya kusudi sana kusafiri toka miisho yote ya Dunia kwenda Yerusalemu ili kupata elimu ya Mungu zaidi. Badala ya chafuko na utaratibu wa kuhusiana na binadamu usio na haki na utawala wa haki, kutakuwa na kanuni moja ya sheria"Sheria na neno la Bwana"Vitatamkwa na Kristo toka Yerusalemu."Mataifa yote yatakwenda makundi makundi"kwenye vipindi vya mafunzo haya, yanadokeza kuwa hii nia ya watu wote kutafuta elimu ya kweli juu ya Mungu itapunguza mabishano yaliyozaliwa nayo kati ya mataifa, kama yafanyavyo kati ya mtu na mmoja mmoja wanaojitoa wenyewe kujipatia elimu kama hii katika maisha haya.

Namna hii ya mataifa kufurika katika mji wa Yerusalemu ni moja na picha inayoonyesha katika

Isa. 60: 5

, ambapo Wayahudi "Wanakwenda pamoja"na watu wa mataifa (wasio wayahudi) kumwabudu Mungu katika mji wa Yerusalemu. Habari hii inaungana kikamilifu na unabii ulio katika

Zekaria. 8: 20 -23:

-

“Itatokea halafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa miji mingi; wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya ! twendeni zetu kwa haraka

(Zek. 14: 16

mwaka kwa mwaka) tuombe fadhili za Bwana , na kumtafuta Bwana wa majeshi; mimi nami nitakwenda. Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana ….. watu kumi, wa Lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; Naam, wataushika wakisema, tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi”

Hii inaumba picha ya watu wa Uyahudi kufanywa"Kichwa na sio mkia" wa mataifa, kwa ajili ya kutubu kwao na utiifu

(K/Torati 28:13)

;Mpango wa Mungu kwa Wayahudi wa wokovu wakati huo utakubalika na kila mtu. Kutokujua huku miongoni mwa Wakristo wa wakati ule ule basi utafikia mwisho mara moja. Wakati huo watu kwa shauku watajadili mambo haya. Kwa kusudi kwamba waweze kuwaambia wayahudi,"tumesikia ya kwamba Mungu yu pamoja nanyi”. Mazungumzo yatakuwa mambo ya kiroho wakati huo, kuliko mizuka inayojaa fikira za ulimwengu uliopo.

Kutolewa sharti kubwa kwa utauwa, halishangazi kuwa Kristo "atafanya hukumu katika mataifa mengi, ….Nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe minundu: Taifa halitainua upanga juu ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe"

(Isa. 2:4

).

Mamlaka kamili ya Kristo na haki kabisa ya ushupavu wake katika mabishano utasababisha mataifa kwa hiari kubadili zana za kijeshi na kuwa vyombo vya kilimo na kuacha mafundisho yote ya kijeshi. "Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi"

(Zab. 72:7)

. Kwa kiroho wakati huo atakuwa na hali ya juu, na heshima watapewa walio na sifa ya upendo wa Mungu, huruma na haki. Ni tofauti na wakati uliopo wa kuwa juu wenye kiburi, wenye kujidai na wachoyo wenye tamaa ya kuwa maarufu.

Hiari ya kufua"Mapanga kuwa majembe"itakuwa sana sehemu kubwa ya mabadiliko kwa kilimo kitakachokuja duniani, kwa toleo la dhambi ya Adamu, ardhi ililaaniwa kwa ajili yake

(Mwa. 3: 17 -19)

, pamoja na matokeo ya jitihada kubwa inatakiwa kwa sasa ili kupata chakula. Katika ufalme wa Mungu"utakuwepo wingi wa nafaka katika ardhi juu ya milima - yaani sehemu kame; na matunda yake yatawaya -waya kama (mazao)

Lebanoni"

(

Zab. 72:16)

."Alimaye atamfikilia avunae,naye akanyagae zabibu atamfikilia apandae mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu"

(Amosi. 9:13)

, ndivyo ardhi itakuza hali ya uzaaji, na kupunguza laana iliyotamkwa Edeni juu ya ardhi

Bidii hii kubwa kwa kilimo itahusisha watu wengi. Unabii na ufalme unatoa fikira ya kuwa watu watarejea kujitosheleza, kwa mtindo wa maisha ya kulima: -

“Wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, chini ya mtini wake; wala hakuna mtu atakayewatia hofu"

(Mika. 4:4)Huku kujitosheleza kutashinda matumizi mabaya yaliyo ndani ya mfumo wowote wa ajira ya kazi kwa ajili ya kupata pesa. Kutumia maisha yote kufanya kazi ya kuwafanya watu wengine watajirike wakati huo itakuwa ni jambo lililopita.

“Watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine …. Wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. Hawatajitaabisha kwa kazi bure ……"

(Isa. 65: 21 -23).Isaya 35: 1 -7

ina unabii usio na kifani jinsi nchi kame itakavyobadilika, ikisababisha kuwa katika hali ya shangwe na kufurahisha karibu ikitiririka toka kwenye nchi, kwa sababu ya kuwa na raha na zaidi maisha ya kiroho kwa wale watendaji : "Nyika …. Pata furahi ….. jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua … na kufurahi , naam, kwa shangwe na kuimba …….. maana katika nyika maji yatabubujika, na vijito jangwani. Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji na nchi yenye kiu itakuwa chemi chemi za maji”. Hata tendo la asili la kushambuliana kati ya wanyama litaondolewa:"mbwa mwitu na mwana kondoo watalisha pamoja”, na watoto wataweza kucheza na nyoka

(Isa. 65:25; 11: 6 - 8).Kwa njia hiyo hiyo Laana iliyowekwa juu ya wanyama kwa ukubwa itapunguzwa, Hivyo na tokeo lililowekwa juu ya wanadamu nalo pia litapunguka.

Ufu. 20: 2,3

inasema hivi kwa lugha ya ishara ya Ibilisi (

dhambi na matokeo yake

) "Kufungwa"au kuzuiwa, kwa kipindi cha millenia yaani miaka elfu. Maisha ya kuishi yataongezeka, hivyo basi mtu akifa mwenye miaka 100, atadhaniwa bali kuwa ni mtoto

(Isa. 65:20)

Wanawake watapata uchungu mdogo wakati wa kujifungua mtoto

(mst. 23

). "Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na viziwi masikio yao yatazibuliwa. Mtu aliye kilema ataruka -ruka kama ndama, na ulimi wake aliye bubu utaimba"

(Isa. 35: 5,6)

. Hii itakuwa kwa sababu ya kuwepo vipawa vya Roho

(Ebra. 6:5).Ufalme waMungu kwa nguvu hauwezi kukaziwa mno kama kuonekana kama kisiwa chenye joto jingi peponi, ambacho watu wenye haki watafurahia kwa namna hii watu wanavyofurahia kuota jua baada ya kuogelea katikati ya kujivunia maumbile. Kusudi la msingi wa Ufalme wa Mungu ni kutoa utukufu kwa Mungu, hata dunia itajawa na utukufu wake"Kama maji yaifunikavyo bahari"

(Habakuki 2:14)

. Hii ni shabaha aliyokuwa nayo Mungu tangu asili:"Kama niishivyo, dunia nzima itajaa utukufu wa Bwana"

(Hes. 14: 21)

. Utukufu kwa Mungu maana yake ni kwamba wakaazi wa dunia watatoa shukrani, Sifa na mfano ulio kiini cha tabia yake; kwa kuwa ulimwengu utakuwa katika hali hii, Mungu atafanya nayo dunia inayoonekana itoe utukufu pia. Hivyo"Wapole watairithi nchi (Katika ufalme wa Mungu) Watajifurahisha kwa wingi wa amani (ya kiroho)" (

Zaburi 37:11)

, kuliko kufurahia maisha ya starehe. Hao"Walio na njaa na kiu ya haki …. Watashibishwa"

(Math.5:6).Wazo tu la kuwa na uzima wa milele katika ufalme mara nyingi limetumika kama 'kuwavuta kuwapa zawadi’ ya kuwashawishi watu kwenye mapenzi ya Ukristo. Ingawa hivyo, wakati huu wa kuwa nalo sisi, karibu ni la kufuata kama matokeo kwa sababu yetu ya kweli kuwamo katika ufalme ambao ni kwa kumtukuza Mungu. Ni kwa muda gani litasalia nasi baada ya sisi kubatizwa, ufahamu wetu kwa hili daima utakua. Kwa maandishi, kuishi miaka kumi tu kwa furaha ya utimilifu kabisa na dhamiri njema na Mungu lngekuwa bora kuliko maisha haya ya shida. kama hali hii yenye utukufu itadumu mielele akili peke yake inapanuka mno, na kuchukuliwa kupita upeo wa fahamu ya mwanadamu.

Hataitazamwapo kidogo zaidi kwa maneno ya kimwili, kuwa katika ufalme wa Mungu kuwe ni kusudi kuu letu kudharau faida za ulimwengu na kujikusanyia vitu vya mwilini. Badala ya kuwaza mno u karibu wa wakati ujao Yesu alishauri,"Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa"

(math. 6:30 -34)

Kila kitu ambacho sasa tunaweza kufikiri na kujitahidi hakilinganishwi na utimilifu wa mwisho wa kuwamo katika ufalme wa Mungu.

Tunatakiwa kutafuta "haki (

ya Mungu)

”, yaani kujaribu kukuza upendo wa tabia ya Mungu, ambayo maana yake ni kwamba tunataka kuwa katika Ufalme wa Mungu kwa sababu haki itatukuzwa humo, kwa sababu tunataka kwa uadilifu tuwe kamili kabisa kuliko tu kwa sababu sisi wenyewe’ tunataka kuepuka mauti na kuishi maisha ya raha milele.

Tumaini la Injili lote pia mara nyingi limeonyeshwa kwa njia ambayo inatazamisha ubinafsi wa mwanadamu. Ni dhahiri kusudi letu la kuwamo kwenye ufalme wa Mungu kwa ukubwa linahitilafiana toka siku hadi siku. Tunachodokeza hapa ni wazo la ukamilifu; kipaumbele chetu ni

kujifunza injili na kuonyesha kuwa tunaitii kwa ubatizo kutokana na wazo lenye upendo wa kumtii Mungu. Kuthamini kwetu tumaini ambalo Mungu anatoa, na sababu zetu hasa za kutosha kuamo katika Ufalme, zitakua na kukomaa baada ya ubatizo wetu.
2010-07-19 18:44 Читать похожую статью
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • © Помощь студентам
  Образовательные документы для студентов.